Monday, 20 October 2014

USIKATE TAMAA KWA KUUPIMA UMBALI KWA MACHO. Anza kwa kusimama, tembea huku ukiwa na matumaini. Mdogo mdogo na nia ndani yake utafika..

nimekaa hapa chini nikawaza,,,, hili jani la mti lipo mbali sana, hata nimesimama sijaweza kulifikia. mmh hapana.. nia yangu ni kulishika hili jani...

nimejaribu kuruka kidogo nikaruka tena, hatimae nikaweza kuligusa jani. na hivi ndivyo maisha yalivyo. ukipima kwa macho na kuwaza kwa akili yenye udhaifu unapata asilimia nyingi za kukata tamaa. iwapo utasimama na kuanza kutafuta namna ya kupata unachohitaji ni rahisi kufikia malengo. 

No comments:

Post a Comment