MAHITAJI;
Unga wa mchele
Uji mzito wa Unga wa ugali
Hiriki
mayai kama 2
koroga unga wa mchele kwa kiasi unacho taka kutokana na hitaji lako.
changanya na hiriki zilizotwangwa, pia changanya na Mayai katika uji wa unga wa mchele.
changanya na uji wa unga wa ugali ulioukoroga na kisha kupoa kuwa wabaridi., tia uji huo katika uji wa mchele na kisha koroga pamoja na baadae tia amira na ufunike ili mchanganyiko huo uumuke.
kama unavyo vyungu vya kupikia viandae kwa kuvifuta kwa mafuta tayari kwa matumizi.
baada ya unga wako kuumuka andaa jiko hata kama ni la umeme weka moto kiasi ili uweze kupata pishi lisiloungua. kwa kutumia vyungu utapika kwa kawaida tu..
lakini pia unaweza kutumia frampeni kama hauna vyungu.
weka mafuta ya kupikia na kisha pata moto weka uji huo mzito na ufunike na bakuri ya chuma ili uji usitapakae kwenye frampeni na baada ya dakika kadhaa funua na utazame.
kama kitakuwa katika muonekano mzuri basi geuza ili kitumbua kiive upande wa pili.
hivi ndivyo unavyoweza kupika kitumbua kwa kutumia frampeni.
No comments:
Post a Comment