Tuesday, 21 October 2014

story. EMANUEL EDNA MACHA


Sawa tukifika Singida tutapumzika kidogo kabda ya kuendelea na safari na tutakapo kuwa tunarudi tutakupa taarifa mapema ili ujiandae. Edna alimwambia mama yake huku akiwa amempakata mtoto wake Emanuel. Wote wakiwa wamechoshwa na safari na kuamua kusinzia ndipo ukatokea mshindo mkubwa ulionyesha  hali haikuwa shwari.

Mara lile basi likaanza kupoteza mwelekeo na hatimae likafika katika mteremko mkali uliopelekea basi lile kupinduka na kuburunguka mara tatu.  lilipo enda kutulia, ndipo baadhi ya abiria waliweza kuokolewa na watu ambao walishuhudia ajali ile.

Abiria wengi walipoteza maisha na baadhi ya abiria walipata majeraha na kukimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu. Alionekana mtoto mdogo akirandaranda huku akilia, mtoto huyo alionekana kukosa muelekeo na hakuna aliyemjari. Ijapokuwa kuna wakati alilia na kukaa chini huku akiokata vitu chini na kuvitia mdomoni lakini hakuna hata mtu aliyeshughulika nae.

************************************************************************************
VASILISA;

Alikuwa miongoni mwa abiria ambaye alikaa jirani kabisa na emanuel pamoja na wazazi wake, japokuwa alikuwa amejeruhiwa sehemu za ubavuni na kupelekea kupata maumivu makali lakini aliweza kuelewa kila kinachoendelea pale katika eneo la tukio. 

Vasilisa alimuomba mmoja kati ya waokoji kumsaidia kumbeba yule mtoto na awaongoze hospital ili wakapate huduma ya kwanza kwani yeye alijihisi kuumia sana sehemu za ubavuni. Aliweza kupata msaada kama alivyotaka na ndipo walifikishwa hospitalini na kufanyiwa vipimo vyote.

Mtoto emanuel alionekana kutokuwa na tatizo lolote ila kwa upande wa vasilisa alionekana kumivywa na kitu kigumu kilichopelekea kumpa maumivu ya ndani kwa ndani na mbaya zaidi Mimba yake iliharibika na hapo ilionyesha wazi kwamba hatoweza kuzaa tena kutokana na kizazi chake kupata hitirafu.

Pole vasilisa Mrembo; ulichokitarajia hakitawezekana tena kwani hadi kizazi chako kimepatwa na matatizo hivyo basi unapaswa kumshukuru Mungu kwa hili. Yalikuwa maneno ya daktari katika kumfariji Vasilisa alipokuwa akilia kwa uchungu.

daktari aliendelea kumbembeleza vasilisa, Mtunze sana huyu kijana wako ndio mtoto pekee atake weza kukufariji na kukufanya uwe na furaha. hakuna njia yoyote ingine. ( maskini daktari alijua mtoto  emanueli ni mtoto wa vasilisa).**************************************************************
*******************************************************************************

Vasilisa hakuwa na neno la kuzungumza kwa wakati huo, Akili yake ilikuwa imeisha choshwa na maelezo ya daktari, aliwaza vitu vingi bila kupata jibu, hakujua mmewe atapokea vipi taarifa ya daktari pindi atakapo muelezea kwamba hatoweza kupata mtoto tena. ilikuwa ngumu zaidi pale alipoanza kufikiria furaha aliyoipata kwa kipindi kifupi baada ya kufunga ndoa na mmewe. hakika vasilisa alichoka zaidi kwani hakujua Hatma ya ndoa yake.

Mlango unafunguli taratibu na daktari anaingia ndani akiwa na mtoto emanueli huku akimbembeleza.. Nenda kwa mama,,,, haya nenda kamuonyeshe mama,,, poleee polee baba. vasilisa ananyanyuka na kumtazama emanueli ambaye kasimama huku analia tuu.. akainama na kumchukua emanueli , pole baba, tuone ulipoumia ,, ok pole,, asante daktari. aliendelea kumbembeleza emanueli mpaka alipopitiwa na usingizi akamlaza taratibu kwa uangalifu ili asimshtue.

bado anajiuliza, kuzaa sitaweza tena na huyu mtoto nae ananipa mtihani sana, sijui wazazi wake walipo, na je wasipopatikana itakuwaje? sitaweza kuwapata ndugu zake mahala walipo, itakuwa jukumu langu kumlea huyu mtoto, sitaweza ruhusu kumwacha akalelewe kwenye vituo vya kulelea watoto yatima wakati mimi sina mtoto. nitamchukua awe wangu hata kama ndoa itakufa potelea mbali.


furaha ya ajabu kwa vasilisa baada ya mume wake kukubali kumpokea mtoto Emanueli baada ya kugundua kwamba ni ngumu kupatikana kwa nduguze kwani mbali ya jitihada walizozifanya ikiwa ni pamoja na kutangaza kwenye vyombo vya habari ndani wa miezi miwili lakini hapakutokea mtu yeyote ambaye alikiri kumfahamu mtoto huyo.

maisha yaliendelea kwa vasilisa na mmewe huku wakimlea emanueli kama mtoto wao pekee. baada ya miaka kadhaa kupita emanueli akiwa na miaka kama 7 siku moja mchana wakiwa wamekaa mezani wanakula ghafla wanasikia geti likigongwa........ hodiii... jamani hodi... hodi humu ndani..........

emanueli anakimbia kwenda kufungua geti huku mama na baba yake wakimfuata nyuma kwenda kushuhudia ni nani anyegonga geti kwa nguvu utazani anakimbizwa huko alikotoka....
ghafla.....!!!!!!!!!!!! nipeshe we mtoto  alaaah.....!!!!!! hapa sio kwenu peke yako hata kelvin nae anahaki ya kukaa kwa raha kama wewe... pisha nipite..... Mwanamke yule akaingia ndani kwa hasira huku akiwa na mwanae kelvin kamshika mkono..

mtoto kelvin anaonekana kama anamiaka minne, ni mdogo kwa Emanuel.

Patric anashanga fujo za mwanamke yule,,,,,,,!!!!!!   huku akiwa na hofu juu ya tukio lile anaanza kwa kumsihi mwanamke yule anakuja kama kiparafumbi kisichokuwa na msimu ...  Prisca taratibu basi hata kama umefikia hatua hiyo ,,, hapa sio nyumbani kwako unatakiwa kuwa na heshima prisca....

mwanamke anakuja juu kwa kumrushia swali bovu bovu Patric.....  heshima gani,,,? huyu mtoto umeniachia toka mchanga wewe na mkeo na huyo mtoto wenu mnaishi kwa raha tu... sikubali Patric shika mwanao naomba niache na maisha yangu. nimechoka kuwa mtumwa.. hebu niache niangalie maisha yangu...


Patric nilikubali kuzaa na wewe kwa kuwa ulinambia kwamba huyu mkeo hana uwezo wa kuzaa.. sasa mbona humuachi bado unaangaika nae humu ndani.. si umwache nije mie ninayeweza kukupa watoto wengi...

Patric alipandwa na hasira na kumjibu mwanamke yule kwa jeuri... siwezi muacha mke wangu kwa ajili yako wewe.. naomba elewa kuwa nilikuomba tuzae kwa makubaliano ya mimi kupata mtoto na sio kuacha mke wangu. unaweza muacha kelvin hapa na wewe ukaenda zako... toka haraka ...... tokaaaaa haraka Prisca..

prisca aliondoka kwa hasira na kumtelekeza mtoto  na kuondoka zake huku kauli mbaya zikimtoka mdomoni bila kujari watu waliokuwa wakimtazama. kelvin alianza kulia kwa hofu ya kuachwa na watu asio wafahamu, hakuzoea kumuona yeyote kati ya wale walio kuwepo nyumba ile.. Emanuel alimchukua kelvin na kuanza kumbembeleza huku akiamini mto yule atanyambaza pindi usingizi utakapo mchukua ma kumfanya alale. aliondoka na kelvin na kuelekea chumbani kwake na kuwaacha baba na mama yake wakiwa pale mezani .                                                                        


Vasilisa akiwa  kasimama huku akionekana kuchoshwa na kilichotokea aliongea kwa upole,,, Patric hebu nieleweshe tafadhali ni nini hiki kimetokea? mbona sielewi!!! nahisi kama naota tu...

samahani vasilisa haitakuwa busara kuongea hapa kwani emanuel apaswi kujua chochote juu ya haya.. hebu vuta subira hata kesho Mungu akijaria tunaweza kuongea..

vasilisa alishindwa kuendelea kula kwani akili ilikuwa imesha vurugukika.. aliwaza mengi juu ya ugeni ule. mmmh.. vasilisa mimi hata sijui nimemkosea nini Mungu wangu., sina uwezo wa kuzaa tena hili mosi,,,, Mume wangu kaenda kuzaa nje na mama wa mtoto ndio yule mcharuko kwisha kazi,,, sijajua Emanuel akija kujua kwamba sisi sio wazazi wake itakuwaje.. Mbona mtihani ninao.. sijajua mme wangu atazaa mara ngapi nje au ndio ndoa yangu imefika mwisho...!! hata sijui mwisho wa ndoa yangu ni upi au ndio mateso yameisha anza kunikaribia.. huku akilia kwa uchungu chumbani kwake vasilisa alikuwa kajiinamia pembeni ya kitanda chake wakati mmewe patric alikuwa bado mezani akitafakari ni vipi ataanza kuongea na mkewe.

Patric aliwaza mengi sana,, atumie nguvu kueleweka au amweleze kwa upole ili waweze kuelewana.
masaa yalizidi kwenda,, mwisho usingizi ulimchukua na kulala pale pale huku kichwa amekiegemeza juu ya meza..

huku chumbani nako vasilisa alilia mpaka akashikwa na usingizi na kulala moja kwa moja.. majira ya saa nane usiku patric alishituka na kukuta bado yupo sitting room. alinyanyuka kwa uchovu na kuelekea chumbani..

next day.

Emanuel akiwa anakunywa chai huku kabeba begi lake tayari kwa kwenda shule ghafla anasikia kelvin akilia chumbani. alitua kikombe na kuelekea chumbani.. unalia nini kev.?
namtaka mama kev..
nyamaza mama kevi atakuja baadae kukuchukua.

Emanuel aliongea maneno yale kwa ajili ya kumfariji kev kwani alikuwa hajui kama mama kev angerudi kumchukua mwanae kwa siku ile.

Patric alikuwa ameisha jiandaa tayari,, akiwa anatoka ,, ghafla vasilisa anamuuliza.....

sasa Patric unaniachaje na huyu mtoto? je mama yake akija kumchukua itakuwaje?

kuhusu hilo usijari,, kwanza ukisikia mtu anagonga getini usifungue bila kumuuliza yeye ni nani... na ukishajua ni yeye wala usimruhusu kuingia mwambie anipigie simu mimi.... sawa?

sawa. lakini huyu mtoto atalia sana leo. bado mdogo na mazingira bado mageni kwake,,,,
patric hakujibu, alifungua mlango na kuondoka na emanuel,,

wakiwa njiani, Patric anaonekana kuwa na mawazo mengi sana yaliyopelekea wote wawe kimya ndani ya gari.

ghafla Emanuel anamkumbusha baba yake, baba nishushe kituo kinachofuata na pia usisahau pesa ya mtihani mwisho leo kulipia. Patric hakujibu kitu bali alisimamisha gari na Emanueli akashuka.........
... Nakutakia siku njema,,, hivyo ndivyo Patric aliweza kumuaga Emanuel......... asante baba kwako pia.

akiwa njiani emanueli aliwaza jinsi Prisca alivyowavuruga Usiku uliopita. alimuona ni mwanamke asiye na huruma hata kidogo kwa kiumbe chake, alichukua simu yake na kumpigia prisca.. prisca hakupokea simu ya patric...

Patric aliamua kutoa uwamuzi wa kwenda kutoa taarifa polisi kwaajiri ya usalama wake.
baada ya kuandikisha maelezo Patric alielekea ofisini kwake moja kwa moja.
jioni alirudi nyumbani na kumkuta mkewe Vasilisa macho yamevimba kwa kulia....

nini shida mama?Patric aliuliza
mtoto ....Vasilisa alijibu
mtoto kafanyaje..?
amegoma kula kanywa maziwa tu. hata sijui nifanyeje nahisi mtihani mkubwa sana. atateseka sana kwa kukaa na njaa.

emanueli aliposikia kelvine hajala chakula zaidi ya kunywa maziwa alisikia huruma sana. akambeba na kutoka nae nje.
Emanuel alimpenda kelvine ghafla...alimnunulia chips na mayai na juice,, hakujua kwamba ulikuwa udhaifu wa kelvine.

baadae walirudi nyumbani na kukuta baba na mama yao wamekaa sebuleni kimya...........


vipi mbona kafurahi kelvine? mama yake alihoji kwa kushangaa
nimemnunulia chips na juice kala kamaliza kila kitu. Emanuel alijibu na kuwafanya wazazi wao wapate matumaini na kugundua namna ya kuweza kuishi na mtoto yule hasa kwa upande wa chakula. vasilisa alipanga kumnunulia kelvine kile ambacho angependa kula hata kama bajeti itakuwa haitoshi nyumbani basi wao wangebangaiza ilimradi tu mtoto apate kile anachotaka.


No comments:

Post a Comment