Wednesday, 29 October 2014

NAIANDIKA HII KWAKO

MAHITAJI;

 Unga wa mchele
Uji mzito wa Unga wa ugali
Hiriki
mayai kama 2

koroga unga wa mchele kwa kiasi unacho taka kutokana na hitaji lako.

changanya na hiriki zilizotwangwa, pia changanya na Mayai katika uji wa unga wa mchele.

changanya na uji wa unga wa ugali ulioukoroga na kisha kupoa kuwa wabaridi., tia uji huo katika uji wa mchele na kisha koroga pamoja na baadae tia amira na ufunike ili  mchanganyiko huo uumuke.


kama unavyo vyungu vya kupikia viandae kwa kuvifuta kwa mafuta tayari kwa matumizi.


baada ya unga wako kuumuka andaa jiko hata kama ni la umeme weka moto kiasi ili uweze kupata pishi lisiloungua. kwa kutumia vyungu utapika kwa kawaida tu..


lakini  pia unaweza kutumia frampeni kama hauna vyungu.

 weka mafuta ya kupikia na  kisha pata moto weka uji huo mzito na ufunike na bakuri ya chuma ili uji usitapakae kwenye frampeni na baada ya dakika kadhaa funua na utazame.

kama kitakuwa katika muonekano mzuri basi geuza ili kitumbua kiive upande wa pili.

hivi ndivyo unavyoweza kupika kitumbua kwa kutumia frampeni.

SOMETIMES


Monday, 27 October 2014

NILIFURAHI SANA KUONANA NA DADA ZANGU, RAFIKI NA NDUGU ZANGU.. SASA NAAMINI; MILIMA HAIONANI LAKINI BINADAMU TUNAONANA.


Furaha iliyoje kuonana nanyi tena. kutoka mbata primary school mpaka leo bado tunapendana. hakika was a wonderful day. NICE TO MEET YOU GUYZ

Wednesday, 22 October 2014

NIDHAMU NA KUJITUMA NDIO NJIA PEKEE YA KUWEZA KUJIONGEZEA KIPATO

Nikiwa na staff wenzangu katika semina ya maboresho kazini.

THINKING ABOUT*************

MAISHA NI WEWE NA HAKUNA MTU MWINGINE KATIKA MAISHA YAKO.

Nina imani sana na hii kauli... Kuna age inafika unatakiwa kujitambua na kukubali.  Maisha ni mimi na hakuna mtu mwingine katika maisha yangu.

Anza kwa kujitambua na kupanga mikakati. duu...!!!!!  hakuna mtu anaweza kukuambia maisha ni mepesi au alipo anzia ni karibu, HAPANA kila umuonae ana history yake mpaka kufikia hapo alipo.




 Twende kaziiiii....

kazi ni mpango mzima. Pigana kupata unacho stahiki kukipata.. Tabasamu pia ili kuifanya akili yako ikae sawa.

NI TIMU NZIMA YA MISS CHANG'OMBE ILIPO TEMBELEA KAMPUNI YA KIWANGO SECURITY GUARDS (T) LTD. KIWANGO SECURITY ILIKUWA MIONGONI MWA WADHAMIN WA MASHINDANO HAYA.

SITTI ABAS MTEMVU NDIE ALIYEIBUKA MSHINDI SIKU HIYO.. YANAYOZUNGUMZWA SASA KUHUSU MREMBO HUYU YANASIKITISHA SANA.

1. ALIPOVAA TAJI LA MISS CHANG'OMBE HAMKUYAJUA ?

2. KWANINI WATANZANIA UWA ATUPENDI KUONGEA UKWELI?

3. KWANINI WATANZANIA WENGI UWA ATUPENDI MAENDELEO .


NI VIZURI KUCHUKUA HATUA TOKA AWALI.  KAMATI HUSIKA YA MISS TANZANIA ILIKUWA NA VIGEZO NA INAELEWA KILA KITU KUHUSU MREMBO HUYU.

HIVI INAWEZEKANA KWELI KAMATI ILIKUWA HAIJUI INACHO KIFANYA?

HIVI ANAE STAHILI KULAUMIWA NI MISS TANZANIA AU KAMATI ILIYOMCHAGUA?

TWENDENI MBELE NA PIA TURUDINI NYUMA KABDA YA KUWEKA VITU HADHARANI.

Tuesday, 21 October 2014

story. EMANUEL EDNA MACHA


Sawa tukifika Singida tutapumzika kidogo kabda ya kuendelea na safari na tutakapo kuwa tunarudi tutakupa taarifa mapema ili ujiandae. Edna alimwambia mama yake huku akiwa amempakata mtoto wake Emanuel. Wote wakiwa wamechoshwa na safari na kuamua kusinzia ndipo ukatokea mshindo mkubwa ulionyesha  hali haikuwa shwari.

Mara lile basi likaanza kupoteza mwelekeo na hatimae likafika katika mteremko mkali uliopelekea basi lile kupinduka na kuburunguka mara tatu.  lilipo enda kutulia, ndipo baadhi ya abiria waliweza kuokolewa na watu ambao walishuhudia ajali ile.

Abiria wengi walipoteza maisha na baadhi ya abiria walipata majeraha na kukimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu. Alionekana mtoto mdogo akirandaranda huku akilia, mtoto huyo alionekana kukosa muelekeo na hakuna aliyemjari. Ijapokuwa kuna wakati alilia na kukaa chini huku akiokata vitu chini na kuvitia mdomoni lakini hakuna hata mtu aliyeshughulika nae.

************************************************************************************
VASILISA;

Alikuwa miongoni mwa abiria ambaye alikaa jirani kabisa na emanuel pamoja na wazazi wake, japokuwa alikuwa amejeruhiwa sehemu za ubavuni na kupelekea kupata maumivu makali lakini aliweza kuelewa kila kinachoendelea pale katika eneo la tukio. 

Vasilisa alimuomba mmoja kati ya waokoji kumsaidia kumbeba yule mtoto na awaongoze hospital ili wakapate huduma ya kwanza kwani yeye alijihisi kuumia sana sehemu za ubavuni. Aliweza kupata msaada kama alivyotaka na ndipo walifikishwa hospitalini na kufanyiwa vipimo vyote.

Mtoto emanuel alionekana kutokuwa na tatizo lolote ila kwa upande wa vasilisa alionekana kumivywa na kitu kigumu kilichopelekea kumpa maumivu ya ndani kwa ndani na mbaya zaidi Mimba yake iliharibika na hapo ilionyesha wazi kwamba hatoweza kuzaa tena kutokana na kizazi chake kupata hitirafu.

Pole vasilisa Mrembo; ulichokitarajia hakitawezekana tena kwani hadi kizazi chako kimepatwa na matatizo hivyo basi unapaswa kumshukuru Mungu kwa hili. Yalikuwa maneno ya daktari katika kumfariji Vasilisa alipokuwa akilia kwa uchungu.

daktari aliendelea kumbembeleza vasilisa, Mtunze sana huyu kijana wako ndio mtoto pekee atake weza kukufariji na kukufanya uwe na furaha. hakuna njia yoyote ingine. ( maskini daktari alijua mtoto  emanueli ni mtoto wa vasilisa).**************************************************************
*******************************************************************************

Vasilisa hakuwa na neno la kuzungumza kwa wakati huo, Akili yake ilikuwa imeisha choshwa na maelezo ya daktari, aliwaza vitu vingi bila kupata jibu, hakujua mmewe atapokea vipi taarifa ya daktari pindi atakapo muelezea kwamba hatoweza kupata mtoto tena. ilikuwa ngumu zaidi pale alipoanza kufikiria furaha aliyoipata kwa kipindi kifupi baada ya kufunga ndoa na mmewe. hakika vasilisa alichoka zaidi kwani hakujua Hatma ya ndoa yake.

Mlango unafunguli taratibu na daktari anaingia ndani akiwa na mtoto emanueli huku akimbembeleza.. Nenda kwa mama,,,, haya nenda kamuonyeshe mama,,, poleee polee baba. vasilisa ananyanyuka na kumtazama emanueli ambaye kasimama huku analia tuu.. akainama na kumchukua emanueli , pole baba, tuone ulipoumia ,, ok pole,, asante daktari. aliendelea kumbembeleza emanueli mpaka alipopitiwa na usingizi akamlaza taratibu kwa uangalifu ili asimshtue.

bado anajiuliza, kuzaa sitaweza tena na huyu mtoto nae ananipa mtihani sana, sijui wazazi wake walipo, na je wasipopatikana itakuwaje? sitaweza kuwapata ndugu zake mahala walipo, itakuwa jukumu langu kumlea huyu mtoto, sitaweza ruhusu kumwacha akalelewe kwenye vituo vya kulelea watoto yatima wakati mimi sina mtoto. nitamchukua awe wangu hata kama ndoa itakufa potelea mbali.


furaha ya ajabu kwa vasilisa baada ya mume wake kukubali kumpokea mtoto Emanueli baada ya kugundua kwamba ni ngumu kupatikana kwa nduguze kwani mbali ya jitihada walizozifanya ikiwa ni pamoja na kutangaza kwenye vyombo vya habari ndani wa miezi miwili lakini hapakutokea mtu yeyote ambaye alikiri kumfahamu mtoto huyo.

maisha yaliendelea kwa vasilisa na mmewe huku wakimlea emanueli kama mtoto wao pekee. baada ya miaka kadhaa kupita emanueli akiwa na miaka kama 7 siku moja mchana wakiwa wamekaa mezani wanakula ghafla wanasikia geti likigongwa........ hodiii... jamani hodi... hodi humu ndani..........

emanueli anakimbia kwenda kufungua geti huku mama na baba yake wakimfuata nyuma kwenda kushuhudia ni nani anyegonga geti kwa nguvu utazani anakimbizwa huko alikotoka....
ghafla.....!!!!!!!!!!!! nipeshe we mtoto  alaaah.....!!!!!! hapa sio kwenu peke yako hata kelvin nae anahaki ya kukaa kwa raha kama wewe... pisha nipite..... Mwanamke yule akaingia ndani kwa hasira huku akiwa na mwanae kelvin kamshika mkono..

mtoto kelvin anaonekana kama anamiaka minne, ni mdogo kwa Emanuel.

Patric anashanga fujo za mwanamke yule,,,,,,,!!!!!!   huku akiwa na hofu juu ya tukio lile anaanza kwa kumsihi mwanamke yule anakuja kama kiparafumbi kisichokuwa na msimu ...  Prisca taratibu basi hata kama umefikia hatua hiyo ,,, hapa sio nyumbani kwako unatakiwa kuwa na heshima prisca....

mwanamke anakuja juu kwa kumrushia swali bovu bovu Patric.....  heshima gani,,,? huyu mtoto umeniachia toka mchanga wewe na mkeo na huyo mtoto wenu mnaishi kwa raha tu... sikubali Patric shika mwanao naomba niache na maisha yangu. nimechoka kuwa mtumwa.. hebu niache niangalie maisha yangu...


Patric nilikubali kuzaa na wewe kwa kuwa ulinambia kwamba huyu mkeo hana uwezo wa kuzaa.. sasa mbona humuachi bado unaangaika nae humu ndani.. si umwache nije mie ninayeweza kukupa watoto wengi...

Patric alipandwa na hasira na kumjibu mwanamke yule kwa jeuri... siwezi muacha mke wangu kwa ajili yako wewe.. naomba elewa kuwa nilikuomba tuzae kwa makubaliano ya mimi kupata mtoto na sio kuacha mke wangu. unaweza muacha kelvin hapa na wewe ukaenda zako... toka haraka ...... tokaaaaa haraka Prisca..

prisca aliondoka kwa hasira na kumtelekeza mtoto  na kuondoka zake huku kauli mbaya zikimtoka mdomoni bila kujari watu waliokuwa wakimtazama. kelvin alianza kulia kwa hofu ya kuachwa na watu asio wafahamu, hakuzoea kumuona yeyote kati ya wale walio kuwepo nyumba ile.. Emanuel alimchukua kelvin na kuanza kumbembeleza huku akiamini mto yule atanyambaza pindi usingizi utakapo mchukua ma kumfanya alale. aliondoka na kelvin na kuelekea chumbani kwake na kuwaacha baba na mama yake wakiwa pale mezani .                                                                        


Vasilisa akiwa  kasimama huku akionekana kuchoshwa na kilichotokea aliongea kwa upole,,, Patric hebu nieleweshe tafadhali ni nini hiki kimetokea? mbona sielewi!!! nahisi kama naota tu...

samahani vasilisa haitakuwa busara kuongea hapa kwani emanuel apaswi kujua chochote juu ya haya.. hebu vuta subira hata kesho Mungu akijaria tunaweza kuongea..

vasilisa alishindwa kuendelea kula kwani akili ilikuwa imesha vurugukika.. aliwaza mengi juu ya ugeni ule. mmmh.. vasilisa mimi hata sijui nimemkosea nini Mungu wangu., sina uwezo wa kuzaa tena hili mosi,,,, Mume wangu kaenda kuzaa nje na mama wa mtoto ndio yule mcharuko kwisha kazi,,, sijajua Emanuel akija kujua kwamba sisi sio wazazi wake itakuwaje.. Mbona mtihani ninao.. sijajua mme wangu atazaa mara ngapi nje au ndio ndoa yangu imefika mwisho...!! hata sijui mwisho wa ndoa yangu ni upi au ndio mateso yameisha anza kunikaribia.. huku akilia kwa uchungu chumbani kwake vasilisa alikuwa kajiinamia pembeni ya kitanda chake wakati mmewe patric alikuwa bado mezani akitafakari ni vipi ataanza kuongea na mkewe.

Patric aliwaza mengi sana,, atumie nguvu kueleweka au amweleze kwa upole ili waweze kuelewana.
masaa yalizidi kwenda,, mwisho usingizi ulimchukua na kulala pale pale huku kichwa amekiegemeza juu ya meza..

huku chumbani nako vasilisa alilia mpaka akashikwa na usingizi na kulala moja kwa moja.. majira ya saa nane usiku patric alishituka na kukuta bado yupo sitting room. alinyanyuka kwa uchovu na kuelekea chumbani..

next day.

Emanuel akiwa anakunywa chai huku kabeba begi lake tayari kwa kwenda shule ghafla anasikia kelvin akilia chumbani. alitua kikombe na kuelekea chumbani.. unalia nini kev.?
namtaka mama kev..
nyamaza mama kevi atakuja baadae kukuchukua.

Emanuel aliongea maneno yale kwa ajili ya kumfariji kev kwani alikuwa hajui kama mama kev angerudi kumchukua mwanae kwa siku ile.

Patric alikuwa ameisha jiandaa tayari,, akiwa anatoka ,, ghafla vasilisa anamuuliza.....

sasa Patric unaniachaje na huyu mtoto? je mama yake akija kumchukua itakuwaje?

kuhusu hilo usijari,, kwanza ukisikia mtu anagonga getini usifungue bila kumuuliza yeye ni nani... na ukishajua ni yeye wala usimruhusu kuingia mwambie anipigie simu mimi.... sawa?

sawa. lakini huyu mtoto atalia sana leo. bado mdogo na mazingira bado mageni kwake,,,,
patric hakujibu, alifungua mlango na kuondoka na emanuel,,

wakiwa njiani, Patric anaonekana kuwa na mawazo mengi sana yaliyopelekea wote wawe kimya ndani ya gari.

ghafla Emanuel anamkumbusha baba yake, baba nishushe kituo kinachofuata na pia usisahau pesa ya mtihani mwisho leo kulipia. Patric hakujibu kitu bali alisimamisha gari na Emanueli akashuka.........
... Nakutakia siku njema,,, hivyo ndivyo Patric aliweza kumuaga Emanuel......... asante baba kwako pia.

akiwa njiani emanueli aliwaza jinsi Prisca alivyowavuruga Usiku uliopita. alimuona ni mwanamke asiye na huruma hata kidogo kwa kiumbe chake, alichukua simu yake na kumpigia prisca.. prisca hakupokea simu ya patric...

Patric aliamua kutoa uwamuzi wa kwenda kutoa taarifa polisi kwaajiri ya usalama wake.
baada ya kuandikisha maelezo Patric alielekea ofisini kwake moja kwa moja.
jioni alirudi nyumbani na kumkuta mkewe Vasilisa macho yamevimba kwa kulia....

nini shida mama?Patric aliuliza
mtoto ....Vasilisa alijibu
mtoto kafanyaje..?
amegoma kula kanywa maziwa tu. hata sijui nifanyeje nahisi mtihani mkubwa sana. atateseka sana kwa kukaa na njaa.

emanueli aliposikia kelvine hajala chakula zaidi ya kunywa maziwa alisikia huruma sana. akambeba na kutoka nae nje.
Emanuel alimpenda kelvine ghafla...alimnunulia chips na mayai na juice,, hakujua kwamba ulikuwa udhaifu wa kelvine.

baadae walirudi nyumbani na kukuta baba na mama yao wamekaa sebuleni kimya...........


vipi mbona kafurahi kelvine? mama yake alihoji kwa kushangaa
nimemnunulia chips na juice kala kamaliza kila kitu. Emanuel alijibu na kuwafanya wazazi wao wapate matumaini na kugundua namna ya kuweza kuishi na mtoto yule hasa kwa upande wa chakula. vasilisa alipanga kumnunulia kelvine kile ambacho angependa kula hata kama bajeti itakuwa haitoshi nyumbani basi wao wangebangaiza ilimradi tu mtoto apate kile anachotaka.


AMETUMIA KITU KIGUMU KUEGEMEZA KICHWA CHAKE LAKINI NDANI YA MOYO WAKE AMEJAA IMANI KUBWA SANA . IJAPO KUWA KWA KUTAZAMA PICHA ANAONEKANA KUCHOSHWA NA YANAYOMSIBU..






TUNAEGEMEZA VICHWA VYETU KATIKA VITU LAINI SANA.. LAKINI NDANI YA MIOYO YETU KUMEOTA MAGUGU NA MIZIZI YA UKATILI.

KWA YULE MWENYE HOFU YA MUNGU TU NDIE ATAKAYEWEZA KUSHINDA VITA DHIDI YA UKATILI.

wakati mwingine watoto hupenda kuona ni jinsi gani wazazi wao tunawajali na kutambua uwepo wao. nilifanya hivi kumfariji kijana wangu kwani asubuhi kabda sijaenda kazini aliniambia anaumwa na niliporudi jioni nikamkuta kakasirika sana.. oooh no my boy.. nikaanza kumpiga picha wee mpaka akafurahi.

watoto ni faraja ndani ya nyumba.



Moja ya vitu ambavyo navipenda nikiwa safarini. ni ule wakati wa kupata chochote.. napenda kununua vitu vidogo sana na kinywaji hiviii.... Pia napenda kuwa na tunda Apple.. sikosi big G.

kwa vile huwa sipendi kusinzia.. basi mimi sikosi vijarida kwenye mkoba wangu..

Rafiki wewe unapendaje ukiwa safarini.

Kuna wakati mtu upenda kukaa mwenyewe kwa furaha yako na kupata mda mzuri wa kufikiri mambo yako binafsi pasipo kumshirikisha mtu. sometimes unahisi kuwa mwenyewe tuu.. uwaze hili na lile kwa upana zaidi.

Aliamua kutoka mwenyewe kupata upepo na utulivu wa akili.. nimependa muonekano wakeee...

 chukua hii wewe piaaaa.....




NI MAZAO YANAYO PATIKA NDANI YA TANZANIA.
 Ni fresh kutoka shambani.


Monday, 20 October 2014

NI KATIKA HARAKATI ZA KUKUWEKA SALAMA NA HURU MDA WOTE. LINDA NA KIWANGO SECURITY GUARD. ni kampuni ya ulinzi iliyopo maeneo ya KAWE BEACH.

 TUNDURU:

Ni moja ya safari zake katika kukuhakikishia wewe unaelindwa na KIWANGO SECURITY GUARDS (T) LTD upo salama.
FIRE RESPONSE:

0715 - 900 000
0716 - 777 779
+255 222 860 777
+255 713 213 060
Alarm Response, CCTV monitoring
access Control electric Fencing, Perimeter Beams Guarding Division.
gate and Garage Automation Gms Camera. Data card system Panic Alarm Response.



Mbali ya huduma ya ULINZI kiwango security ni watengenezaji wa fenicha kama unavyoona pichani


info@kiwangosecurity.com
kiwango@yahoo.com

Ni moja kati ya semina za kuboresha utendaji kazi.


hatuwezi kupendana bila kufahamiana. na Atutaweza kwenda mbele bila kushikamana.

nimeipenda hii status nikaona si vibaya kama nikishare nawewe.

ni miaka mingi sana walivalia hivi .. kwa siku hizi inakuwa na mtazamo tofauti.


zamani miaka ya 1960 walivaa mavazi haya.

NDANI YA JOINT PUB

Tulimaanisha Hakuna matata Ni Upendo zaidi. ...!!!!!!!!!


ndivyo tulivyoweza kuonyesha upendo SERENGETI FIESTA 2014 ndani ya banda la joint Pub

Ilibamba ile mbaya.. watu walifurahi na kupart .. Fiesta 2014.ilikuwa ki upendo zaidi. 
mbali ya kufurahi nanyi hapa Viwanja vya Leaders pia tuna wakaribisha  Joint Pub iliyopo maeneo
ya KIGAMBONI karibu na MIKIDADI beach. 


Ni Shiiiiidaaa.



ndivyo tulivyoweza kuonyesha upendo. SERENGETI FIESTA 2014 katika banda la joint Pub

NYAM NYAM NYAM........ MISHIKAKI

Hata mboga pia uchangia kufanya upate hamu ya kula chakula..

1. utumbo wa nyama ya ng'ombe
2. majani ya kunde
3. kitunguu maji
4. nyanya
5. nyanya chungu
6. Tui zito la nazi

hivi ndivyo nilivyoipika mboga hii. . .

mimi nilikula kwa ugali tena nilienjoy sana jaribu na wewe uone radha yake

USIKATE TAMAA KWA KUUPIMA UMBALI KWA MACHO. Anza kwa kusimama, tembea huku ukiwa na matumaini. Mdogo mdogo na nia ndani yake utafika..

nimekaa hapa chini nikawaza,,,, hili jani la mti lipo mbali sana, hata nimesimama sijaweza kulifikia. mmh hapana.. nia yangu ni kulishika hili jani...

nimejaribu kuruka kidogo nikaruka tena, hatimae nikaweza kuligusa jani. na hivi ndivyo maisha yalivyo. ukipima kwa macho na kuwaza kwa akili yenye udhaifu unapata asilimia nyingi za kukata tamaa. iwapo utasimama na kuanza kutafuta namna ya kupata unachohitaji ni rahisi kufikia malengo. 

URAFIKI WA UTOTO UNAVYOKUWA. lakini times come age fulani uwenda wasikumbukane tena. yote haya husababishwa na purukushani katika maisha.


 
 michezo ya watoto katika kipindi chao cha kufurahia maisha yao ya watoto.. hapo utaita weee wala hakusikii hata chakula anaweza kusamehe ilimradi tu asiache kucheza.

 kila mtu amepita katika kipindi hiki.. ni wachache sana ambao
mpaka kufikia utu uzima wanakuwa wanafanya mawasiliano. asilimia kubwa  tunapotezana. hali hii ni kwa sababu ya kuhangaika na maisha.