Wednesday, 19 November 2014

INDONESIA

Kipimo cha Bikira kimeorodheshwa kuwa moja ya matakwa ya kuingia kwenye Jeshi nchini Indonesia. Wanawake waliofanyiwa kipimo hicho walisema walipata maumivu na kujisikia kudhalilishwa.

Imeelezwa kuwa Askari wa kike nchini humo walipeleka malalamiko kwa ngazi za juu za jeshi la Polisi bila mafanikio.

Afisa wa Juu wa HUMANI RIGHTS WATCH Nisha Varia amesema; kipimo hicho ni unyanyasaji na kinawadhalilisha wanawake.
Polisi Mjini Jakarta wametakiwa kufuta kipimo hicho na kukipiga marufuku nchi nzima. Polisi nchini humo wadai kuto fanya kipimo hicho kwa sasa kwa kuwa kimepigwa marufuku,  hata hivyo hakuna ushahidi wa kutosha uliothibitishwa kusitishwa kwa zoezi hilo kwani katika tovuti yake eneo la kazi tangazo la tarehe 05/11/2014 imeelezwa kuwa wanawake wanaotaka kuwa Polisi wanapaswa kujaribiwa kama wana Bikira.

sababu za kufanya kipimo hiki ni kwamba hawahitaji wanawake wasio na bikira kwani wana wafananisha na makahaba.


Swali: Je mwanamke bikira anafanya kazi kwa ufanisi kuliko yule asiye na bikira? Na je asiye na bikira hana adabu kuliko yule mwenye bikira?

Toa maoni yako


No comments:

Post a Comment